Header Ads

Mimi kama Amiri Jeshi Mkuu najisikia raha sana na furaha kubwa ninapokuwa na wanajeshi-Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  amesema kuwa yeye kama askari aliyeiva huwa hatikisiki hata kwa upepo wa aina gani. 

Rais Magufuli  leo Novemba 10, wakati akikagua magari ya JWTZ yaliyoandaliwa kwa ajili ya ununuzi wa korosho. 

"Mimi kama Amiri Jeshi Mkuu najisikia raha sana na furaha kubwa ninapokuwa na wanajeshi kama nyinyi . Mimi ni askari niliyeiva huwa sitikisiki hata kwa upepo wa aina gani na mara nyingi waliojaribu kunitingisha walitingisika wenyewe, lakini nafahamu kuna Jeshi la wananchi wa Tanzania ambao kwenye historia yao tangu lilipoanza halitingishiki na wala halitegemei kutikisika wala kamwe halitatikisika katika maisha yote tangu Jeshi hili lianzishwe," amesema Rais Magufuli.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.