Header Ads

Mo Dewji akutana na viongozi wapya wa SimbaWiki moja baada ya klabu ya Simba kufanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi watakaoingoza kwa miaka 4 ijayo, uongozi huo leo umekuatana na mwekezaji wa klanu hiyo Mohammed Dewji.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo haijafafanua zaidi juu ya kilichojadiliwa katika kikao hicho ambacho kimekutanisha kwa mara ya kwanza wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba SC.
''Leo Jumamosi Novemba 10, 2018 kimefanyika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ambacho kwa mara ya kwanza wajumbe wa bodi hiyo ambao walichaguliwa katika uchaguzi mkuu wa klabu uliofanyika wiki iliyopita wameshiriki'', imeeleza taarifa hiyo.
Simba ilifanya uchaguzi wake Novemba 4, 2018 na kumchagua Swedi Mkwabi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo huku Crescentius Magori akitangazwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Simba Sports Club.
Mo Dewji ameweka kwenye kalbu hiyo kwa kununua asilimia 49 ya hisa huku asilimia 51 zikibaki kwa wanachama wengine.
 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.