Header Ads

Monalisa apongezwa


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo amempongeza Msanii wa Filamu, Yvonne Cherrie (Monalisa)kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda.

Fissoo amempongeza msanii huyo jijini Dar es Salaam alipokutana naye na kuzungumzia masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.

Aidha Fissoo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii na kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.