Header Ads

Mzee akilimali atanganza kugombea

Mzee Akilimali Atangaza Kuchukua Nafasi ya Manji Yanga
Imeelezwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, ametangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya klabu hiyo.

Taarifa zinasema kuwa Akilimali amefikia hatua hiyo kutokana na namna klabu hiyo ilivyo kwenye hali ngumu hivi sasa.

Mzee huyo amesema tayari kuna wanachama wa Yanga waliojitokeza kumlipia fomu hivyo wakati ukishafika ataenda kuchukua.

Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshawekea msisitizo wake kuwa uchaguzi wa Yanga utafanyika Januari 13 mwaka kesho.

Wakati huo pande zote mbili kati ya Yanga na TFF wamekubaliana kusimamia kwa pamoja uchaguzi huo kupitia kamati zao.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.