Header Ads

Rais magufuli akagua magari ya jeshi la wananchi JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo Jumamosi, Novemba 10, 2018 amekagua magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ.

Magari hayo yanaweza kutumika kubebea Korosho katika mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) iwapo wanunuzi wa zao hilo hawatazinunua baada ya siku ya Jumatatu saa 10:00 kama alivyoagiza jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitoa siku 4 kuanzia jana Ijumaa hadi Jumatatu, Novemba 12, kwa wanunuzi wote korosho kupeleka barua Ofisini kwake kuonyesha tani wanazohitaji, lini watazichukua.

Majaliwa alisema baada ya hapo hawatanunua tena korosho hizo, zaidi watafutiwa usajili wa ununuzi wa zao hilo.

Hii ni kutokana na sintofahamu kwenye minada ya zao hilo kuu la biashara Tanzania.Advertisement

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.