Header Ads

SIKUMBUKI NI LINI NIMEENDA SALUNI

Davina Afuata Nyayo za Wolper na Shilole
MSANII wa kitambo kwenye tasnia filamu nchini, Halima Yahaya ‘Davina’ amesema kuwa kwa sasa hakuna staa ambaye anayejielewa na ‘anafuga kucha’ zaidi ya kuchakarika na kazi za kumuingizia kipato.

Akizungumza na Amani, Davina alisema kuwa amesahau hata lini ameenda saluni kwa ajili ya kutengeneza kucha kama ilivyokuwa huko nyuma maana kutwa anashinda jikoni kwa ajili ya kupika chakula cha

kuwauzia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). “Sidhani kama sasa hivi yupo staa anakumbuka kwamba kuna kwenda saluni kuoshwa au kupakwa rangi kama ilivyokuwa huko nyuma, kwa kweli mimi ni jiko na mimi kila wakati,” alisema Davina.

Davina amefuata nyayo za wasanii wa kike waliojikita kwenye ujasiriamali akiwemo Shilole ambaye ana mgahawa, Wolper ambaye anashona nguo mbalimbali na wengineo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.