Header Ads

Stamina afichua siri ya mtoto wa mtarajiwaMKALI wa muziki wa  kufokafoka kutoka pembezoni mwa Milima ya Uluguru iliyopo Mji Kasoro Bahari, Morogoro, Boniveture Kabogo ‘Stamina’ amefichua siri ya mtoto mtarajiwa ikiwa imepita miezi michache tangu afunge ndoa.
Akipiga stori na Showbiz, Stamina alisema anatarajia kupata mtoto wakati wowote kuanzia sasa na kwamba siku hizi teknolojia imerahisisha mambo ambapo wanandoa mnaweza mkapanga muda gani mpate mtoto na awe wa jinsia gani, huku akifunguka zaidi kuwa endapo atapata mtoto wa kiume atamuita Lionel na kama akiwa wa kike atamuita Antonella.
“Kila kitu kinaenda sawa na muda wowote mke wangu anaweza akanipa mtoto, sababu ya kuwapa majina hayo ni kwamba nampenda sana Lionel Messi wa Barcelona, hivyo mwanangu wa kiume nitamuita Lionel kuonyesha ni kiasi gani namkubali yule mchezaji,” alifichua siri Stamina. Stamina alifunga ndoa na mkewe, Veronica mwezi Mei, mwaka huu mkoani Morogoro

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.