Header Ads

Unajua watu wamekuwa wakihoji sana sababu ya mimi kumuoa mama Diamond-Shamte

Shamte Afunguka  Kuoa  na Kuishi kwa Mama Daimond
MAISALA Shamte ‘Anko’ ambaye ni mume wa mama wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ amefungukia madai ya kwamba hana nyumba na ndiyo maana anaishi nyumbani kwa mkewe, Madale jijini Dar.  Shamte amesema kuwa, anashangazwa na maneno hayo kwani ana kwake lakini anaishi Madale kwa kuwa kote ni nyumbani kwake.

Amesema, kikubwa anachokitaka kutoka kwa mkewe ni heshima ya mume na anaipata hivyo suala la kuishi kwake siyo ishu.

“Unajua watu wamekuwa wakihoji sana sababu ya mimi kumuoa mama Diamond na kuishi kwake lakini wanasahau kuwa zote ni nyumba, siku tukiamua kukaa Bunju (kwake) tutakaa na siku tukiamua kukaa Madale tutakaa kama tunavyokaa sasa, ishu si makazi bali ni heshima ya mume kwani napikiwa, nafuliwa na huduma zote napata,” alisema Anko.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.