Header Ads

Wakandarasi wazawa watakiwa kuwa wepesi


Wakandarasi Wazawa nchini Watakiwa kuwawepesi kukamilisha Miradi wanayopewa na serikali Kwa Wakati na Kiwango chenye ubora ili kujijengea sifa kwa serikali na kuamika.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, Hamphrey Polepole, wakati wa kukagua miradi ya maendeleo inasimamiwa na serikali mkoani Mara.

Akiwa wilayani Serengeti, ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti na kutoa maagizo ya kuboreshwa mfuko wa bima ya afya na utoaji huduma bora kwa wananchi, ambapo pia alizungumza na wafanyabiashara na wazee wa wilaya hiyo, kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili.

Akiwa katika daraja la Mto Mara linalotenganisha Wilaya ya Tarime na Serengeti Mkoani Mara, kukagua utekelezaji wa Ilani,  pamoja na kuridhishwa na hatua ya ujenzi chini ya Mkandarasi Mzawa, amewataka wakandarasi wazalendo kutekeleza miradi wanayopewa na serikali kwa kiwango na kuikabidhi kwa wakati ili kujenga sifa na uwezo wa kuaminiwa na serikali.

Amesema Kuchelewesha miradi na kuijenga chini ya kiwango, imekuwa ni miongoni mwa changamoto inayowakabili baadhi ya wakandarasi wazalendo, hali inayopelekea kukosa sifa na vigezo vya kupewa kazi za ujenzi wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samwel Kiboye, amewataka watendaji wa serikali kushirikiana na chama tawala ili kuimarisha utendaji kazi kwa wananchi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.