Header Ads

WANANCHI KATA YA UHAMBULE, WANGING’OMBE HAWAJARIDHIKA NA MRADI WA TASAFNJOMBE:Wananchi wa kijiji cha Msimbazi kata ya Uhambule wilayani Wanging’ombe mkoa wa Njombe hawajaridhika na ujenzi unaofanywa na mkandarasi anayejenga madarasa mawili na vyoo kwa ajili ya shule ya msingi ya mfano ya Msimbazi ambao unafadhiliwa na Mpango wa Kunusuru kaya masikini (TASAF) baada ya kutumia nguvu kazi zao za kusomba mawe na kuchanga zaidi ya shilingi milioni tisa kuunga mkono mradi wa shule, huku kiasi cha shilingi milioni 65  zikiwa zimetolewa na Tasaf, lakini hali hairidhishi baada ya kutumia kiasi cha shilingi milioni 45 hadi sasa….

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ametaka kupata majibu sahihi ya gharama halisi zilizotumika kwenye ujenzi wa majengo ya shule ya mfano na kutoa agizo la kufanya ufuatiliaji kwa karibu ya juu ya matumizi ya pesa zilizokwisha tumika hadi sasa pamoja na michango ya nguvu za wananchi  zaidi ya shilingi milioni  tisa .

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Msimbazi wamezungumza na kituo hiki na kueleza kwamba hawaridhiki na ujenzi uliofanywa na mkandarasi huyo na kuiomba serikali kuchukua hatua stahiki dhidi ya waliofanya udanganyifu..

Naye Afisa Ufuatiliaji wa Mradi wa Tasaf katika Halmashauri za Makambako, Wanging’ombe na Mbarali mkoa wa Mbeya, Edwin Mlowe amewataka wataalam wa halmashauri wanaofanya kazi ya kusimamia miradi ya Tasaf kuacha kukaa maofisini na badala yake ni vyema wakajiridhisha na ujenzi wa miradi inayoibuliwa na wananchi..

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.