Header Ads

Wanaotaka niachane na iyobo watasubiri sana-Auty EzekielSTAA wa filamu kutoka Bongo Muvi, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa amekuwa akisikia fununu kila kukicha kuwa ameachana na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ambaye ni dansa maarufu wa Wasafi Classic Baby (WCB), kusema kuwa wanaosema hivyo watasubiri sana.

Akizungumza na Ijumaa, Aunt alisema afikiri katika dunia hii hata kama unapenda na mtu kwa kiasi gani hamuwezi kuishi bila kutokea ugomvi wowote kwa sababu wao sio malaika lakini wanapogombana wanayamaliza na maisha yanaendelea kama kawaida lakini inavyoonekana kuna watu wanataka kuona penzi lao likisambaratika kabisa.
“Nafikiri wanaosema tumeachana watasubiri sana kama kugombana hakuna wanaoishi kama malaika, kwa sababu wote ni binadamu lakini hatuna ugomvi endelevu, yule ni mzazi mwenzangu na wanaosubiri tuachane tutawaacha mbali sana,” alisema Aunt.

Maneno yalizuka zaidi staa huyo kuachana na mzazi mwenzake baada ya yeye na mtoto wake pamoja na ndugu zake walipoenda kusherekea sikukuu yake ya kuzaliwa nchini Dubai, huku Iyobo akiwa amebaki nchini.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.