Header Ads

WCB wafunguka haya kuhusu Hawa

WCB Yatoa Tamko Lingine Kuhusu Hawa
Meneja wa Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ amesema msanii Hawa Said ambaye yupo nchini India kimatibabu, anayo nafasi ya kujiunga na kundi lao la Wasafi Classic Baby (WCB) endapo atapenda kufanya hivyo Mungu akimjalia kurudi salama nchini.

Akizungumza na Risasi Jumamosi jana, Babu Tale alisema kwa sasa hali ya Hawa inaridhisha ila bado hajajua siku ya kurudi hadi wapate ruhusa kutoka kwa madaktari na kuongeza kuwa, akisharudi na afya yake kuimarika akiamua binafsi kufanya tena muziki ni sawa na wanamkaribisha WCB.

“Tunashukuru Mungu kwa muujiza alioutenda maana ilikuwa ni hatua ngumu mno lakini kafanya wepesi mpaka sasa hivi hali yake siyo mbaya inaridhisha ila kurudi tutasema muda ukifika. Na akisharudi akimaliza kujiuguza kama akitaka kuendelea na muziki hayo ni matakwa yake, nafasi ipo na tunamkaribisha WCB,” alisema Babu Tale.

Wakati huohuo Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram alidai kuwa atamuwezesha pesa ya kufanyia biashara iwapo atampa wazo anataka kufanya nini.


“Nafarijika kuona unatabasamu sasa nitafurahi kusikia wazo zuri la biashara toka kwako nikuwezeshe,” aliandika Diamond kwenye ukurasa wake.

Hawa aliondoka nchini Oktoba 13, mwaka huu kwenda nchini India ikielezwa anakwenda kutibiwa tatizo la ini lakini alipofika nchini humo ilibainika kuwa ana tatizo la moyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.