Header Ads

Ally Kiba aanza mazoezi Coastal Union

Mchezaji wa timu ya Coastal Union Ally Kiba ameanza mazoezi na timu yake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kiba ambaye ni mwanamuziki na mdhamini wa klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu alikuwa nje ya kambi kwa muda kutokana na majukumu yake ya kikazi.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema amefanikiwa kumpa programu maalumu Kiba ambayo itamfanya kuwa bora zaidi hasa kwa kuwa hajacheza muda mrefu akiwa na timu yake.

"Muda mwingi Kiba amekuwa kwenye majukumu yake ila kwa sasa amerejea kwenye kazi yake atafanya kazi na wachezaji wenzake na ameshaanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbeya City," alisema.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.