Header Ads

Ambokile awaburuza Makambo, Okwi na Kagere

Mshambuliaji wa timu ya Mbeya, City Eliud Ambokile leo amefikisha bao lake la 9 kwenye ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya African Lyon mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya.

Ambokile amezidi kuonyesha umahiri wake wa kucheka na nyavu na kuwaacha washambuliaji wa Simba na Yanga Herieter Makambo, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere ambao ni wageni.

Makambo, Okwi na Kagere wote wana mabao 7 baada ya kucheza mechi 13 kwenye ligi kuu huku Mbeya City wakiwa wamecheza michezo 15.
Ligi kuu imeendelea leo katika viwanja tofauti ambapo timu 8 zilikuwa kazini kusaka pointi tatu timu 6 zimefanikiwa kukamilisha dakika 90 huku timu 2 zikishindwa kutokana na hali ya hewa.

Lipuli na Biashara United zimecheza kwa muda wa dakika 26 bila kufungana dakika 64 zilizobaki watamalizia kesho kutokana na mvua kubwa kunyesha wakati wa mchezo uwanja wa Samora.

Matokeo kwa mechi ambazo zimkekamilisha dakika 90 ni kama ifuatavyo:-

Mbeya City 4-1, African Lyon uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kagera Sugar 1-0, Alliance uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Ndanda 0-0 Mbao, uwanja wa Nangwada Sijaona, Mtwara

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.