Header Ads

Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mpenzi wakeJeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba,linamshikiria mwanamke mmoja aliejulikana kwa jina Mwana Kombo Ramadhani Bakari kwa mahojiano maalumu mara baada kutokea kwa kifo cha mpenzi wake ambacho kimetokea kwa Utata.

Akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Madungu Kamanda wa Polisi Mkoa huo Hassan Nassir Ali alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Mwanakombo Ramadhan Bakar anaetokea Mkoa wa Tanga (26).

Alieleza Jeshi la Polisi liliona ni bora kumshikilia mwanamke huyo na kumuhoji ili kubaini kiini cha mauaji ya kijana Samir Abdalla Ali (19) ambae kifo chake kimekuwa na utata mkubwa.

 Alifahamisha kuwa kifo cha marehemu Samir, kilitokea Jumapili baina ya majira ya saa 9:30 alfajiri hadi 12:00 asubuhi nyumbani mwa mwanamke huyo, ambae anadhaniwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na maraehemu.

 “Jeshi la Polisi Mkoa huu linamshikilia Mwanakombo Ramadhani kutokana na mauaji wa kijana huyo ambae kifo chake kimeleta utata, kwani inavyoonekana marehemu alinyongwa na wala hakujinyonga mwenyewe”, alisema Kamanda Nassir kwa uchunguzi wao wa awali.

Hata hivyo Kamanda alisema upelelezi wa shauri hilo unanaendelea kwa kasi kubwa, kwani wamelazimika kuunda timu ya wataalamu wa Jeshi hilo, ambayo inaongozwa na mkuu wa upelelezi wa Mkoa huo.

 Alisema inaimani kuwa, kikosi kazi hicho kitakuwa na majibu ya uhakika, na uchunguuzi utakapokamilika hatua nyengine za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaebainika kufanya tukio hilo.

 “Ombi langu kwa wazazi na walezi wa marehemu wawe wastahamilivu na kuviachia vyombo vya sheria kuendelea na kazi zake,”alifafanua.

 Kuhusu utata ambao Jeshi la Polisi wameuona kufuatia kifo cha marehemu huyo, ni kumkumkuta akiwa ameshafarikia na miguu yake kupinda magoti kama alieuwawa na kisha kwekwa eneo husika.

Tukio jengine ambalo limetokea katika ni la wizi wa kuvunja nyumba na kuiba, lilitokea kijiji cha Masingini Chake Chake, ambapo mtu asiejuilikana alivunja duka na kuiba simu 11 aina ya smat foni zenye thamani ya shilingi milioni 2.3, mali ya Said Salum Ahmed.

 “Hadi sasa bado Jeshi la Polisi linamtafuta aliehusika na tukio hilo, na huku upelelezi ukifanyika kwa kina ili kumpata muhuiska na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhumu hizo,”alifahamisha Kamanda Nassir.

 Tukio jengine ni lile la wizi wa kutumia nguvu, ambapo tukio hilo lililotokezea Wawi Novemba 28, majira ya saa 1:30 usiku, ambapo mtuhumiwa Issa Juma Issa, alimkaba kijana Abraham Benard Mpende.

Kamanda huyo wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba alifafanua kuwa, baada ya mtuhumiwa kumkaba Abraham kisha alimtishia kumchinja kisu, na kufanikiwa kunyang’anya simu na fedha taslim shilingi 50,000.

“Kwa sasa mtuhumiwa huyo wa wizi wa kutumia nguvu, tumeshamkamata na taratibu za kumfikisha mahakamani, zinaendelea ili sheria ichukue mkondo wake,”alifafanua.

Aidha kwenye Jeshi hilo la Polisi, kuliripotiwa tukio la kutishia amani, ambapo mtuhumiwa Khamis Salum Ali alimtishia kumuua kwa kumfukuza panga Raya Muhsini Ali mika 42 mkaazi wa Kipapo.

Tukio hilo lilitokea Novemba 28, mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni, ambapo kwa sasa mtuhumiwa huyo yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi na wakati wowote atafkishwa mahakamani.

Akizungumza kesi ambazo tayari zimeshatolewa hukumu Mahakamani Kamanda Nassir, alieleza kuwa kesi iliyokuwa ikimkabili kijana Ali Othman Hamad, ya wizi wa kutumia nguvu, ilitolewa hukumu yake na mshitakiwa huyo alilazimika kutumikia kifungo cha miaka miwili.

 Mbali na hayo lakini pia Kamanda huyo alieleza kuwa kati kati ya wiki iliyomalizika kulitokea ajali ambayo ilisababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine watano wakijeruhiwa.

 Kamanda Nassir, alisema ajali hiyo ilitokea kijiji cha Mtambile Mkoani, ambapo gari ya mizigo aina ya Fuso yenye namba za usajili Z 312 BR  ikitokea Mtambile na kwenda Mkoani, ilianguka na kusababusha kifo cha mtu mmoja na wengine kujeruhiwa

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.