Header Ads

AY yaionya Burundi

Muungano wa Afrika (AU) umeionya Burundi dhidi ya hatua zinazoweza kuhujumu mchakato wa amani baada ya kutolewa waranti wa kimataifa kumkamata rais wa zamani Pierre Buyoya na maafisa wengine 16.

Wanalaumiwa kwa mauaji ya mwaka 1993 ya raia wa kwanza aliyechaguliwa nchini humo ambaye alitoka kabila la Hutu.

Kuuliwa kwa Melchior Ndadaye kulisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kuna hofu kuwa kumlenga Bw Buyoya ambaye ni kutoka kabila la Hutu anayeishi nchini Mali kunaweza kuchangia kuzuka misukosuko ya kikabila.

Zaidi ya watu 300,000 wameuawa kwenye vita ya miaka 12 vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi lenye wahutsi walio wachache na waasi wa Hutu.

Bw Buyoya ambaye alitwaa madaraka mara mbili ndani ya mingo mitatua iliyopita kwa msaada ya jeshi ni mwanadiplomasia anayeheshimiwa barani.

Awali alipinga vikali madai kuwa alihusika kwenye kifo cha Bw Ndadaye.

Buyoya 69, alihusika kwenye mchakato wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongoza kuchaguliwa kiongozi wa zamani wa waasi wa Hutu Pierre Nkurunziza kuwa rais mwaka 2005.

Mchakato wa sasa na wa amani unafuatia ghasia zilizoibuka na uamuzi wa Bw Nkurunziza kuwannia urais kwa muhula wa tatu mwaka 2015.

Alifanikiwa licha ya kushuhudiwa ghasia za kupinga uamuzi huo na jaribio la mapinduzi ambapo mamia ya watu waliuwa na wengine zaidi ya 400,000 kukimbia makwao.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.