Header Ads

Baadhi ya mila na desturi ndio sababu ya kukwamisha mtoto wa kike kupata elimu


MOROGORO:BAADHI ya mila na desturi za wafugaji  hasa jamii ya kimasai zimetajwa kuwa  chanzo cha kukwamisha ndoto za watoto wakike  katika kupata  elimu  hali inayopekea watoto hao  kutofikia malengo waliyonayo ili waweze  kujikwamua  katika wimbi la kuwa  tegemezi
Bi Rebeka Rembile  ni mhanga wa wa mila na desturi hizo anaelezea  changamoto kubwa aliyokutanayao wakati wa safari yake ya kutafuta elimu  ambapo anasema baada ya kuhitimu daraa la saba  alilazimshwa   kuolewa jambo ambalo hakukubaliana nalo yeye pamoja na baba yake  hali iliyolazimu  kutoroshwa katika  familia yake ili aweze kuendelea na masomo.

Nao baadhi ya  wazazi    wamekili  kuwepo kwa mila hizo na  kueleza kuwa   awali  walitambu  kuwa  mototo wa kike akisoma  anaenda kufaidisha jamii nyingine jambao ambalo halina ukweli kama anavyoleza bw . Milya Chapo na Bi Kelyana Kamunyu

Kwa upande wake mwalimu wa  shule ya msingi Mangae  mkondo wa Mkangazi  B w Javan Peter  amesema  changamoto kubwa kwa jamii hiyo ni kuhamahama mara kwa mara  jambo ambalo husabababisha  wanafunzi kuacha shule  ili kuwafuata wazazi wao

Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo Kanisa la Kiinjiri na Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Morogoro  (KKKT) inaendesha mradi wa MASAI  WORK PROJECT ili kuweza kusaidia jamii za kifugaji   kama anavyoeleza katibu wa Dayosisi hiyo bw Allen Kinyamasongo

Mradi huo unendeshwa kwa lengo la kusaidia jamii mbalimbali za  kifugaji kufahamu umuhimu wa elimu na unatekeleza  mkoani Morogoro kwa  unafadhiri wa   kanisa la Finish lutherani Mission

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.