Header Ads

DAWASA yatakiwa kutoa matangazo kwa wananchiWaziri wa Maji profesa Makame mbarawa  ameitaka  mamlaka ya maji safi na maji taka (DAWASA), kutoa matangazo pindi kunapotokea tatizo la kutokuwepo kwa maji ili kuweza kuepusha usumbufu unaoweza jitokeza kwa wananchi kukosa huduma hiyo.
Akizungumza leo na wakazi wa kata ya wazo salasala waziri mbarawa amesema kuwa kuwa ni wajibu kwa mamlaka hiyo kutoa maji masaa 24 na kama kunakuwa na tatizo la kimfumo watoe matangazo ili wananchi waweze kufahamu mapema.
Aidha Mbarawa  amemtaka mkurugenzi wa Dawasa kuongeza vijana  50 Wa kuwaunganishia wananchi maji kutoka  katika mradi wa maji katika tanki la mradi wa salasala .

Wakizungumza na waziri huyo wakazi wa mtaa wa salasala wamesema kuwa wametuma maombi muda mrefu ila bado hawajafungiwa huduma ya
Naye mkurugenzi  wa Dawasa  amewataka wakazi wa salasala kuwa wavumilivu kwani  mradi uko kwenye  majaribio na kuwataka wananchi kujitokeza kuchukua form za maombi ya maji .

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.