Header Ads

Dkt. Shein akaribisha Jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda ya Sharjah


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameikaribisha Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenye Viwanda ya Sharjah kuzichangamkia fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar.

Dk. Shein aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenye Viwanda ya Sharjah ambae pia, ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi Abdallah Sultan Owais akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Uwekezaji, Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) tayari imeweka mazingira mazuri ya kuwekeza hapa nchini na kusisitiza kuwa milango ya uwekezaji ya Zanzibar iko wazi.

Rais Dk. Shein aliueleza uongozi huo wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenye Viwanda wa Sharjah kuwa Zanzibar ina fursa nyingi za kuwekeza katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo sekta ya utalii, viwanda, ufugaji na nyenginezo ambazo Jumuiya hiyo ina uzoefu.

Mbali ya kuitaka Jumuiya hiyo kuja kuekeza Zanzibar, Rais Dk. Shein pia alisisitiza haja ya kuwepo mashirikiano na uhusiano na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenye Viwanda ya Zanzibar huku akisisitiza kuwa Zanzibar iko tayari kufanya kazi na Jumuiya hiyo.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya ufugaji na kusisitiza azma na malengo iliyoweka ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka kwa Kampuni ya Al Rawabi ya Sharjah ambayo tayari imeshapata mafanikio makubwa.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alitoa shukurani na pongezi kwa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum  Makamo wa Rais na Waziri Mkuu wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa juhudi alizozichukua za kuhakikisha Kampuni ya ndege ya Fly Dubai inaleta ndege kubwa tena ya kisasa hapa Zanziba

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.