Header Ads

Faida na hasara za kutumia kitunguu swaumu katika mwili wa binadamu

Kama ulikuwa hujua ni kwamba kitunguu swaumu kina faida zaidi katika mwili wa mwanadamu kuliko hasara, pia kitunguu swaumu ni dawa kama utaamua kukitumia magonjwa kama maumivu ya kichwa, h kizunguzungu, mshinikizo la juu la damu, saratani/kansa, maumivu ya jongo/gout  hutibika kwa kutumia kitunguu swaumu , pia huongeza hamu ya kula.

Zifuatazo ndizo faida za kutumia kitunguu swaumu.
Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.

Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.

Hasara za matumzi ya kitunguu swaumu katika mwili wa mawadamu.
Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu.

Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha

Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.

Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.

Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.

Kumbuka:                                                                                                                               
ZINGATIA:  Kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.