Header Ads

Filamu ya mwisho kucheza Marehemu Masogange kutoka December 15, 2018

Msanii wa Filamu Bongo, Rammy Galis anatarajia kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Hukumu.

Katika filamu hiyo Rammy Galis amecheza na aliyekuwa Girlfriend wake Marehemu Agnes Gerald maarufu kama Masogange.

Sio Masogange pekee yake bali waigizaji wengine wakubwa na wakali wameshiriki kwenye filamu hiyo itakayozinduliwa kwa mara ya kwanza December 15, 2018 City Mall, Dar es Salaam.

Agness alipata umaarufu mkubwa pindi alipotokea katika video ya msanii Belle 9 ambayo ilikwenda kwa jina la Masongange ndipo na yeye kuanza kutumia jina hilo. Masogange alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.