Header Ads

Gigy Money Abariki ndoa ya Mzazi Mwenzake Ataka Matunzo ya Mtoto

Gigy Money Abariki ndoa  ya Mzazi Mwenzake Ataka Matunzo ya Mtoto
BAADA ya kumwagana na kila mtu kushika hamsini zake, hatimaye msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibariki ndoa ya mzazi mwenzake, Moj ambaye hivi karibuni aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanamke mwingine huku akiwa amesindikiza maneno yaliyoashiria kuwepo kwa ndoa yao. Akizungumza na Ijumaa, Gigy alisema kuwa kwa sasa hana tatizo lolote na mzazi mwenzie huyo, hata akiamua kuoa leo yeye hatojali chochote kwa sababu penzi lao liliisha muda mrefu hivyo wamebaki kama wazazi tu.“Hivi unajua mimi na Moj tulishaachana muda mrefu na kama mnavyoona ana mwanamke mwingine na mimi nina mwanaume wangu, kwa hiyo hata akiamua kuoa leo hii sitakuwa na pingamizi lolote ili mradi tu awe anatoa matunzo mazuri kwa mtoto wake,” alisema Gigy.


Gigy na Moj walifanikiwa kupata mtoto mmoja aitwaye Mayra, hata hivyo penzi lao halikudumu kwa muda mrefu kutokana na kila mmoja kuml aumu mwenzake kwamba ni msaliti, hivyo kupelekea kil a mmoja wao kujiingiza kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.