Header Ads

Jafo awataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kutatua kero za wananchiDODOMA:Waziri wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI. Mh Suleman Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa  kwenda kutatua kero za wananchi katika maeneo yao.

Ameyasema hayo wakati akifunga  semina ya wakuu wa mikoa na   na makatibu tawala iliyo fanyika jijini Dodoma Mh Jafo amesema kuwa miongoni wa tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji kwani migogoro hiyo imekuwa ikichukua muda mrefu.

Aidha, Mh Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuweka mikakati mahususi katika kupambana na janga dhidi ya madawa ya kulevya kwani kwani tatizo hilo limekuwa ni kubwa hapa nchini,

katika hatua nyingine Mh Jafo amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya ukusanyaji wa mapato , kwani chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano, imejipambanua katika ukusanyaji wa mapato na  wastani wa mapato yake ni shilingi milioni 800.

Pia, ,Mh jafo amewapongeza wakuu wa mikoa kwa kusimamia vizuri rasilimali ya madini , kwani wakuu wa mikoa wamejitahidi kwa kiwango kikubwa , na wakiendelea kuweka mkazo mkubwa katika kusimamia  rasilimali zote katika maeneo yao wataweza kuisaidia serikali.

akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa, mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema kuwa kwa kiapo chao na maelekezo waliyo pewa  watayafuata na kuyafanyia kazi.

kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala la mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI  Dkt Zainabu Chaula amesema kwa siku tano walizokuwepo kwenye semina hiyo kwaajili ya mafunzo maalumu viongozi hao wameweza kushiriki  kwa ukamilifu.

Hatahivyo, Mh Jafo amewataka wakuu wa mikoa kujiamini na kuwataka makatibu tawala  kusimamia mikioa yao ili mambo yaende vizuri katika maeneo yao.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.