Header Ads

Kamanda wa jeshi la maji la Marekani akutwa amefariki nyumbani kwake

Kamanda wa komandi ya tano wa Marekani Scott Stearney ambaye kituo chake cha kazi ni Bahrein amekutwa amefariki nyumbani kwake nchini Bahrein.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Generali wa komandi hiyo John Richardson, kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema;Admiral msaidizi wa jeshi la maji la Marekani anayesimamia mashariki ya kati amekutwa amefariki kwenye makazi yake.

Richardson, Hakutoa taarifa zaidi kuhusiana na chanzo cha kifo hicho.

Richardson alinukuliwa akisema kwa hatua ilyopo hawadhani kama Kamanda huyo aliuawa, alisema Uongozi wa Bahrein unaendelea na uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.