Header Ads

Majina ya wanawake 100 wenye nguvu zaidi ulimwenguni

Jarida la "Forbes" limeorodheha majina ya wanawake 100 wenye nguvu zaidi ulimwenguni.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewekwa nafasi ya kwanza katika orodha ya wanawake wenye nguvu zaidi ulimwenguni, akifuatiwa na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na kiongozi wa IMF Christine Lagarde.

Mwenyekiti wa "Sabancı Holding" ya Uturuki,Güler Sabancı amechukua nafasi ya 64 katika orodha hiyo.

Baada ya Angela Merkel,Theresa May na Christine Lagarde orodha hiyo inafuatiwa na mwenyekiti wa "General Motors" Mary Barra,meneja mkuu wa kampuni ya uwekezaji wa Fidelity Abigail Johnson,Mwanzilishi na Makamu wa Rais wa Bill & Melinda Gates Melinda Gates,Mkurugenzi Mkuu wa You Tube Susan Wojcicki,Mkurugenzi Mtendaji wa Santander Group Ana Patricia Botin,Afisa Mtendaji Mkuu wa Lockheed Martin Marillyn Hewson na Mtendaji Mkuu wa IBM Ginni Rometty.

Katika orodha ya mwaka huu,majina mapya ishirini ya wanawake katika ulimwengu  wa siasa,biashara na sanaa yameongezwa kati ya wanawake hao mia moja wenye nguvu zaidi duniani mwaka 2018.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.