Header Ads

Mbarawa aliagiza jeshi la polisi kuchunguza watu wanao uhujumu miundombinu ya majiWaziri wa  Maji  na umwangiliaji Prof Makame Mbarawa ameliagiza jeshi la polisi nchini kufanya uchunguzi wa kina  kwa watu wanaohujumu miundombinu ya Maji katika kata ya kiwalani jijin Dar es salaam  kwa kuyachafua.

Prof Mbarawa ametoa kauli hiyo  jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake alipokutana na wananchi wa Kiwalani na Minazi Mirefu kusikiliza kero mbali mbali za maji pamoja na kukagua mabomba yanayotoa maji, Ambapo amesema kwa jambo hilo serikali haiwezi kukaa kimya,huku akivisisitiza vyombo vya usalama vianze kazi  mara moja.

Aidha amewataka watendaji wa Dawasa kuweka vioski ambavyo vitaweza  kuwasaidia wananchi  wasiokuwa na uwezo wa kuunganishiwa maji nyumbani waweze kupata huduma hiyo. Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam_ Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema walitumia nguvu nyingi katika Mradi wa maji kwenye eneo hilo, ambapo wananchi waliwapiga vita na kudai kuwa wanayo maji  huku dawasa ikisisitiza kuweka  maji safi na Salama na siyo ya kwaoNae Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph amesema kuna uwezekana watu kwenye visima ndio wanachafua maji ambapo bomba linalopitisha maji eneo hilo ni jipya na halina hata miezi sita na bomba na pia alijapasuka.


Awali wakitoa malalamiko yao baadhi ya wananchi wa kiwalani wamesema maji machafu yanayotoka yanahatufu Kali mpaka wanashindwa kuelewa nini tatizo, wengine wakidai kuwa  maji yanatoka usiku wanapoamka asubuhi yamekatika na kama mgao basi wajulishwe  kama kuna mgao.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.