Header Ads

Migongano ya maslahi inaweza kukithiri na kuwa makosa ya jinai -Chande
DODOMA:Imeelezwa kuwa kwa miaka miwili mfululizo Tanzania imefanikiwa kuadhimisha siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa kwa lengo la kuhamasisha uadilifu, uwazi, uwajibikaji na utawala bora  Hapa Nchini.

Hayo yamesema na kamishna wa maadili Mh.Jaji Mstaafu  Harold Nsekela katika kuelekea siku ya  maadhimisho ya maadili  na haki za binadamu kitaifa yatakayo fanyika jijini Dodoma ambapo  amesema kuwa kwa miaka miwili mfululizo Tanzania imefanikiwa kuadhimisha siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa kwa lengo la kuhamasisha, uadili, uwazi, uwajibikaji na utawala bora Nchini.
Insert Nsekela

 
Aidha, Nsekela amesema kuwa iliamuliwa  kuwa Taasisi zote za umma , zinashughulikia masuala ya maadili , haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora, mapambano dhidi ya Rushwa , kushirikiana  pamoja katika kuratibu maadhimisho hayo na kwa  mara ya kwanza maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa yalifanyika 2016 Jijini Dar es salaam.


Akifungua mjadala  wa mgongano wa maslahi katika kuelekea siku ya  maadhimisho ya maadili  na haki za binadamu kitaifa Ambaye ndiye Mgeni Rasmi Mh Jaji Mkuu  Mstaafu  Mohamed  Othman Chande  amesema kuwa kuwa kuna migongano ya mslahi yenye madhara na isiyo ya madhara  lakini migongano hiyo ipo ambayo ni mikubwa na mengine midogo na mingine inaweza kukithiri na kuwa makosa ya jinai.


Mh chande ameongeza kuwa mgongano wa maslahi kati ya wajibu wa umma , yanamngoja mtumishi ambaye ana maslahi nayo au ana uwezo binafsi nayo ambayo yanaweza kumshawishi visivyo mtumishi huyo kwenye utendaji au majukumu katika wajibu wake rasmi na hapa anaeleza .


Katika hatua nyingine Mh Chande amesema  kuwa ili kuwe na mgongano wa maslahi ni lazima kuwe na mambo manne ikiwemo maslahi ya msingi na hapa ana fafanua zaidi.


Naye Dkt James Jesse  Mhadhiri  wa  chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)  akitoa mada   ya ulinzi  wa haki za binadamu  na mgango wa maslahi, amesema kuwa kwa mujibu wa shirika la maendeleo la kimataifa UNDP  limeweka misingi tisa ya utawala bora ikiwemo ushirikishwaji.

Akitoa mada juu ya  matumizi mabaya  ya madaraka, mgongano wa Maslahi  na uwepo wa Rushwa Nchini Mkurugenzi wa mashtaka  Bwana Edson Makallo amesema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo ni lazima kuwa na mkakati wa pamoja ili kuweza kukabiliana  hali hiyo.


Hatahivyo mwaka 2017 maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yalifanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 27 Novemba  hadi tarehe 10 Desemba mwaka 2017 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono uamuzi wa serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma, Huku kauli mbiu ya Maadhimisho hayo yakisema ‘’ uthibiti wa mgongano wa mslahi , nguzo muhimu , kujenga utawala bora.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.