Header Ads

Mwanri atoa maagizo kwa wakulima wa pambaSerikali imewataka wakulima wa pamba mkoani Tabora kuhakikisha kila kaya inalima angalau ekari tatu za zao hilo ili kuchochea upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ametoa agizo hilo wakati za ziara ya kuhamasisha kilimo cha pamba katika vijiji 57 vinavyolima zao hilo wilayani Igunga.

Amesema uzalishaji wa pamba kwa wingi utawezesha viwanda vya Manonga na Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora kufanya kazi mwaka mzima kwa kuwa na malighafi ya kutosha kuendesha viwanda hivyo.

Mwanri amesema, uzalishaji wa sasa ni kidogo na kwamba, Wilaya ya Igunga ambayo ni mzalishaji wa zao hilo mkoani Tabora asilimia 50 tu ya ardhi inayofaa kilimo hicho ndiyo inalimwa.

Amesema wakulima wakiweza kulima angalau asilimia 90 ya ardhi inayofaa kilimo cha zao hilo watasaidia kuwepo kwa pamba nyingi ambayo itachochea ujenzi wa viwanda vipya na hivyo kuongeza ajira kwa vijana.

Mwanri amesema uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na Chama Kikuu cha Ushirika Igembensabo mkoani Tabora wako katika hatua ya mwisho ya kuleta matrekta kwa ajili ya kuvipokesha Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS), ili wanachama wake waweze kutumia katika ukodishaji ili walime mashamba makubwa ya pamba na mazao mengine.

Katika hatua nyingine, Mwanri amewataka watumishi wa umma kuwa na mashamba ya mfano ili kuwawezesha wananchi kujifunza kutoka kwao kuhusu kilimo bora na kinachozingatia kanuni za kilimo bora

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.