Header Ads

Nafurahi nimekamilisha hili kwa mama -Dogo Janja


Msanii wa Bongofleva Dogo Janja a.k.a 'Janjaro', amesema baada ya kumkabidhi mama yake nyumba mpya na kumtoa kwenye maisha ya kupanga aliishiwa nguvu na hajasema lolote zaidi ya kila muda kuonekana haamini kilichotokea.

Akiongea na www.eatv.tv    Dogo Janja amesema aliamua kuvaa jukumu la kuwa baba na kupeleka faraja kwa mama yake mzazi baada ya baba yake kufariki miaka miwili iliyopita.
''Ninafurahi nimekamilisha hili ndani ya miaka miwili, nilijjiwekea malengo haya baada ya kufariki kwa baba yangu ambaye daima alikuwa ananisisitiza niwekeze kwenye mali kama ardhi na nyumba, sasa nimemfurahisha mama yangu kiasi kwamba amekosa cha kusema yaani yuko “Too Emotional”, amesema Janjaro.
Dongo Janja amefunguka kuwa yeye aliondoka nyumbani akawaacha wazazi wake wakiwa kwenye nyumba ya kupanga na muda wote alikuwa analala sebuleni lakini leo ametimiza ndoto kubwa ya kuwa na kwao hivyo mama yake ana haki ya kufurahi.
''Mama ana kila sababu ya kufurahi natamani hata baba angekuwepo yeye alikuwa mshauri wangu mkuu lakini hayupo tena tutaendelea kufanya dua tu kwaajili yake maana ndicho anachostahili kwasasa, huwezi kusema utampa pesa au mali'', ameongeza.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.