Header Ads

Pluijm wa Azam FC avurugwa na kocha wa Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameonekana kumvuruga Kocha wa Azam FC, Hans Pluijm kufuatia kumshusha kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara aliokuwa akiongoza.

Yanga kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 38 baada ya kucheza michezo 14 sawa na Azam FC yenye Pointi 36.

Ofisa habari wa Azam FC, Jaffar Maganga amesema kocha Pluijm amejipanga kuhakikisha wanafanya vema katika mechi zote ili kuweza kurejea kwenye nafasi yao kwa kuwapiku wapinzani wao Yanga.

"Mwanzo tulikuwa tukiongoza msimamo wa ligi kwa muda mrefu, lakini kwa sasa Yanga ndiyo inayoongoza baada ya kumaliza viporo vyao, hivyo tunahitaji kujipanga ili kuweza kufanya vyema katika mechi zinazofuata," alisema.

Azam FC leo watashuka dimbani saa moja usiku kuvaana na Mbao FC ya Amri Said, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.