Header Ads

Polisi wataka Waziri mkuu afunguliwe mashtaka

Polisi mjini New Yourk wanawatafuta wapenzi ambao walichumbiana eneo la Times Square siku ya Ijumaa lakini wakapoteza pete iliyoanguka kwenye shimo.

Picha za CCTV zinaonyesha shughuli ya kutoa posa ikienda mrama huku wapenzi hao wakijaribu kuitafuta pete iliyopotea.

Baada ya kuona video hiyo maafisa walifanikiwa kuipata pete, wakaiosha na sasa wanataka kuwapata wenyewe.

Wametoa wito kwa mwanamume huyo kujitokeza.

Video hiyo ilichuliwa muda mfupi kabla ya usiku wa manane na kutolewa na polisi muda mfupi baadaye.

Haikuonyesha wakati mwanamue huyo alitoa posa lakini kile kinaonekana ni wakati akiinama kuitafuta pete hiyo.

Mpenzi wake (ambaye haijulikani ikiwa alikubali posa hiyo) baada ya kugundua kilichotokea anaweka mikono yake kwenye uso wake.

Anainama karibu naye akijaribu kumsaidia kuitafuta bila mafanikio.

Mwanamume huyo kisha analala chini kujaribu kuitafuta pete lakini pia hakufanikiwa kuipata.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.