Header Ads

Uhaba wa maji tarafa ya Wanging'ombe changamoto

picha ya mtandao

NJOMBE:Tatizo la Uhaba wa Maji Katika Tarafa ya Wanging'ombe Mkoani Njombe Limeendelea Kuota Mizizi Kutokana na Ukame Unaosababisha Wakazi Wake Kulazimika Kutumia Maji Machafu Ya Madimbwi.

Miongoni Mwa Wakazi Wanaolalamikia Tatizo la Uhaba wa Maji ni Pamoja na Wakazi wa Kata ya Saja Ambao Wamemtupia Lawama Mbunge Wao Alipofanya Ziara Ya Kikazi Katika Jimbo Lake la Wanging'ombe.


Clever Nywage na Golden Miho  Ni Wakazi wa Saja Ambao Mbele ya Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Mhandisi Gerson Lwenge Wamepata Kuhoji ni Lini Kilio Cha Maji Kitaisha Kwani ni Kipindi Kirefu Wamekuwa Wakiomba Maji bila Mafanikio. 
Pamoja na Ukweli Kwamba Tatizo la Maji ni La Kitaifa Lakini Wakazi Hao Akiwemo Gidion Sapy Ameendelea Kusisitiza Ahadi Ambazo Zimekuwa Hazitekeleziki Juu ya Maji Jambo Ambalo Wanadai Wamekuwa Wakinywa Maji Yanayotumiwa na Mifugo.

Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Mhandisi Gerson Lwenge Pamoja na Wataala wa Maji Toka Halmashauri ya Wialaya Hiyo Wanakiri Kuwapo Kwa Tatizo Hilo Huku Wakisema Serikali Bado Inaendelea Kushughulia Siku Hadi Siku.Mhandisi Mussa Masasi ni Meneja wa Mamlaka ya Maji Wanging'ombe WANGIWASA Ambaye Anakiri Kuwa Kwa Sasa Licha ya Kuwapo Kwa Tatizo la Upatikanaji wa Maji Lakini Limepungua na Bado Kuna Mikakati Mizuri ya Kushughulikia Tatizo Hilo.Kila Pahala Nchini Tanzania Kumeonekana Kuwapo Kwa Malalamiko ya Uhaba wa Maji Jambo Ambalo Serikali Kupitia Bajeti Ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji Inapaswa Kulipa Uzito Suala Hilo Ili Kuondoa Kero Kubwa Kwa Watanzania.
 
Na Amiri Kilagalila 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.