Header Ads

Vijana watakiwa kubuni njia za kujajiri


Vijana waliopata mafunzo ya uongozi wa jamii wametakiwa kutumia changamoto ya ukosefu wa ajira kuwa fursa kwa kubuni njia mbali mbali za kuweza kujiajiri ikiwa pamaoja na kuzitumia mali ghafi zilizowazunguka.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud ametoa wito huo wakati akifunga mafunzo ya siku 4 kuhusu uongozi wa jamii kwa vijana ishirini na tano yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la makao makuu ya bima mpirani maisara Mjini Unguja.

Amesema kuwa suala la ukosefu wa ajira ni tatizo kwa ulimwengu mzima hivyo mafunzo waliyopatiwa wayatumie  kwa kubuni na kupanga mikakatiti ya kuzitumia fursa zilipo nchini ili waweze kujiendesha kimaisha.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameahidi kushirikiana kwa karibu na wahitimu hao wa wamafunzo ya uongozi wa jamii ili kuona mafunzo waliyoyapata wanafanyia kazi kwa vitendo na kuleta mabadiliko kwa jamii hususani vijana wa Mkoa wake.


Mapema wakizungumza katika ghafla hiyo baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata yamewaongezea uwezo na ari kubwa ya kutaka kuleta madiliko ya maendeleo katika jamii iliyowazunguka na kuahidi kufanya kazi kwa mashirikiano ili kuona lengo la mafunzo hayo linafikiwa na kuweza kusaidia vijana wenzao.

Nao wakufunzi wa mafunzo hayo wameeleza kuwa mafunzo kama hayo wameshatoa katika mikoa mbali mbali ya Tanzania ikiwemo Zanzibar,hivyo imeonekana kuna mahitaji makubwa kwa vijana wa zanzibar kwani awali kulikuwa na maombi ya vijana mia moja na kumi na saba na wengi wao wana sifa za kupatiwa mafunzo hayo.


Mafunzo hayo ya uongozi wa jamii yametolewa na taasisi za Green light Foundation,Nama Foundation  na An-Nahl Foundation kwa vijana ili kuwajengea uwezo wa uongozi na kuwa wabunifu katika masuala mbali ya kijamii na kuweza kuleta mabadiliko

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.