Header Ads

Wale wahalifu wanao kuja Dodoma kufanya kazi ya uhalifu hatuna nafasi -MurotoDODOMA:Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limefanikiwa kumkamata  Yona  Julius (32) Mkazi wa Dar es salaam kwa tuhuma za utapeli wa viwanja.

Akizungumza na waandishi wa habari , Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa mtuhumiwa huwa amekuwa  akitapeli  watu kwa kupitia kampuni anayo imiliki inayo julikana kwa jina la vijana kwanza project (VKP) inayo jihusisha na upimaji wa viwanja.Aidha, kamanda  muroto ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani  na kama kuna wapo waliotapeliwa  na mtuhumiwa huyo wajitokeze.

Katika hatua nyingine kamanda muroto  amesema wamemkamata Salum Salim Pwao (31) mkazi wa Tabata Jijini Dar es salaam  kwa kujifanya afisa wa PSSF  anayeshughulikia mafao ya wastaafu , ambapo amekuwa akiwapigia watu simu wastaafu  wanao fuatilia mafao yao na kuwadai fedha kwaajili ya kushughulikia mafao ili yaweze kutoka kwa haraka.
Mbali na hilo mutoro amesema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata  watu wawili maeneo ya kikuyu kwa kosa la kupatikana  na bhangi misokoto 40, kwani watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya aina ya bhangi  ambayo wanaisokota katika karatasi , na watuhumiwa hao ni Shami Jumbe Jebrea (35),Meck Donald Maula (40) wote wakazi wa mtaa wa kivyambwa kikuyu Dodoma na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

kamanda muroto  amesema kuelekea msimu wa christimas na mwaka mpya kumekuwa na matukio mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza hivyo amewataka madereva  wanao endesha  vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani,wajiepusha na mwendo kasi wawapo barabani ili kujiepusha na ajali ambazo sio za ulazima.


Hatahivyo, Kamanda muroto amesema jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linaendelea na operesheni mbalimbali na misako katika maeneo  yote ya mji wa Dodoma na wilaya zake kwa ajili ya kukamata makosa mbalimbali ya uhalifu ili kuifanya Dodoma kwa sehemu salam ya kuishi, kufanya kazi na kufanya biashara kwa watu wote.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.