Header Ads

WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI NA MAUDHUI
DODOMA:WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUZINGATIA KANUNI ZA MAUDHUI YA REDIO NA TELEVISHENI AMBAZO ZINAKATAZA URUSHAJI WA PICHA ZISIZO NA STAHA ZENYE USHAWISHI WA WAZI KWA VIJANA KUJIINGIZA KATIKA VITENDO VYA NGONO KABLA YA WAKATI.

WITO HUO UMETOLEWA NA WAZIRI WA HABARI SANAA UTAMADUNI NA MICHEZO MH HARRISON MWAKYEMBE WAKATI WA KILELE CHA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA KWA MWAKA 2018 KATIKA UMKUMBI WA JAKAYA KIWETE CONVENTION CENTER JIJINI DODOMA.

WAZIRI MWAKYEMBE AMESEMA VYOMBO VYA HABARI VINA JUKUMU LA KUHAKIKISHA VINATENDA MAJUKUMU YANAYOZINGATIA MIIKO YA TAALUMA, SHERIA NA MAADILI.AKIZUNGUMZI KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA WAZIRI MWAKYEMBE AMESEMA TANZANIA NDIO CHIMBUKO LA LUGHA YA KISWAHILI AMBAPO AMESEMA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI PAMOJA NA WIZARA YA HABARI WANAENDELEA KUSHIRIKIANA ILI KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOJITOKEZA ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KATIKA MATAIFA MBALIMBALI ILI KUENDELEZA UZALENDO NA KUWATAKA WATANZANIA KULINDA UTAMADUNI KWA NGUVU ZOTE.

AWALI AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO BI. SUZAN MLAWI AMESEMA KAMPENI YA UZALENDO NI ENDELEVU NA INA LENGO LA KUWAFIKIA ZAIDI WANAFUNZI NA KWAMBA WIZARA YA HABARI SANAA UTAMADUNI NA MICHEZO INA DHAMANA KUWA YA KUSIMAMIA UZALENDO NA MAADILI YA TAIFA KAMA NGUZO MOJAWAPO YA UTAMADUNI WA NCHI NA KATIKA KUTEKELEZA HILO WAMEBUNI SIKU YA UZALENDO INAYOSHEREHEKEWA KILA TAREHE 8 YA MWEZI WA 12.


HATAHIVYO,KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA ILIZINDULIWA MWAKA JANA NA MAKAMU WA RAIS MAMA SULUHU HASSAN NA KWA MWAKA HUU KAMPENI HIYO IMEBEBA KAULI MBIU ISEMAYO “KISWAHILI UHAI WETU,UTASHI WETU”.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.