Header Ads

ady Jaydee kutoa albamu ya nane mwaka huu


Msanii wa Bongo Fleva, Lady Jaydee ameeleza kuwa mwaka huu atatoa albamu yake ya nane tangu kuanza muziki.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo za mapenzi za kuvunjwa moyo, jumbe mbali mbali kuhusu maisha na hata sherehe ila kugusa nafsi ya kila mtu kama alivyopokea maoni.

"Sijasema nimefikia kikomo ila niko tayari kwa Album yangu ya nane mwaka 2019, moto huwa haulali," ameeleza Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Utakunguka November 27, 2017 Lady Jaydee alisaini makataba lebo ya Taurus Musik ambayo itakuwa inasimamia kazi zake kwa kipindi cha miaka mitatu. Moja ya vipengele vya mkataba huo vilivyoorodheshwa ni kuwa msanii huyo kutoa albamu mbili kwa muda huo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.