Header Ads

Binti wa R. Kelly afunguka haya kuhusu baba yake

Binti wa R. Kelly Amkana Baba Yake Sakata la Unyanyasaji Wanawake Kingono
Binti wa msanii maarufu wa muziki Marekani, R. Kelly, Joan Buku Abi Kelly ameamua kuweka wazi hisia zake juu ya sakata la unyanyasaji wanawake kingono linalomkabili baba yake.

Binti huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuwa yeye na mama yake kama familia hawatajiingiza kwenye sakata hilo, kwani R. Kelly amekuwa akiitenga familia yake kwa muda mrefu.


Abi amedai kuwa sakata hilo la unyanyasaji kingono, yeye kama msichana limemuathiri sana anaposikia baba yake amefanya ukatili huo.

Mama mzazi wa Binti huyo mwenye miaka 20, Andrea Kelly ni moja ya watu walioonekana kwenye Docu-series ya ‘Surviving R. Kelly’ akielezea namna alivyonyanyaswa kingono.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.