Header Ads

Bunge laruhusu nchi ya Masedonia kubadili jina lake

Bunge la Masedonia limepitisha mabadiliko ya katiba yatakayoruhusu kubadilisha jina la nchi hio kuwa Jamuhuri ya Mesedonia ya kaskazini.

Ugiriki nchi mwanachama wa NATO na Umoja wa Ulaya ,muda mrefu imekuwa ikipinga jina rasmi la taifa la Masedonia, kwa kuwa kaskazini mwa nchi ya Ugiriki kuna jimbo linaitwa Masedonia.

Pingamizi la Ugiriki ni moja ya sababu ambazo zilikuwa zikiizuia nchi ya Masedonia kujiunga na umoja wa Ulaya pamoja na NATO.

Majadiliano baina ya Masedonia na Ugiriki yalichukua sura mpya baada ya serikali mpya ya Skopje kuamua kulifanyia kazi suala hilo ili iweze kujiunga na jumuiya hizo mbili.

Suala la jina limekuwa kipangamizi kwa Masedonia kujiunga na Umoja wa Ulaya na NATO tangu nchi hiyo ipate uhuru wake mnamo mwaka 1991.

Kutambaulika kwa taifa la Masedonia kulikamilka rasmi mwezi April mwaka 1993 baada ya nchi wanachama wa Umoja wa mataifa kukubali azimio la kuikubali nchi hio kama taifa huru na mjumbe wa Umoja wa Mataifa. Kutokana na shinikizo la Ugiriki nchi hio ilisajiwa na Umoja wa mataifa kwa jina la "Former Yugoslav Republic of Macedonia (FYROM)"

Ukiachilia mbali mgogoro uliopo baina ya Athens na Skopje, mataifa mengi ukijumuisha Uturukiinalitambua taifa hilo kama Masedonia.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.