Header Ads

Dkt Kigwangala amkumbuka Ruge-Leo nimeamka nakukumbuka. Nakuombea dua, upone haraka

Kigwangala Amkumbuka Ruge  Amuombea Apone Haraka
Waziri wa Maliasilii na Utalii, Dkt. Dkt. Hamisi Kigwangalla amemtakia heri Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu.

Dkt. Hamisi amenukuu maneno ya Ruge Mutahaba ambayo aliwahi kuyatoa siku za nyuma.

"Mara nyingi wanaokupenda hawasemi, na wanaokuchukia hawakujui. Bahati mbaya sana, wanaichukia perception, lile wazo tu," Dkt Kigwangalla amemnukuu Ruge.

"Leo nimeamka nakukumbuka. Nakuombea dua, upone haraka mtu mwema," ameeleza Dkt. Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ruge Mutahaba alitoa kali hiyo mwaka 2015 katika mahojiano na Mtangazaji Salama Jabir kwenye
kipindi chake Mkasi kilichokuwa kikiruka EATV kwa wakati huo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.