Header Ads

Dkt Mahenge atoa maagizo kwa wazazi wenye watoto walio faulu kujiunga na kidato cha kwanza

DODOMA:Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith mahenge amewaagiza wazazi wa watoto wote ambao wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu kuhakikisha hawaendi mahali popote bali wasubiri kwenda shuleni wakati wowote ndani ya wiki hizi mbili.

Dkt mahenge ametoa agizo hilo alipotembelea wilaya ya kongwa kukagua miradi katika Nyanja ya elimu na sekta ya kilimo ambapo amesema wanafunzi wote waliofaulu mkoani Dodoma watapewa vyumba na watasoma.

Aidha dk mahenge ameridhishwa na utendaji kazi wa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya kongwa kwa maandalizi ya kupokea wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza.

Dkt mahenge amewaomba viongozi hao kuanza maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa muhula ujao mapema kwa kuwa wanajua ratiba za kimasomo kila mwaka mwezi wa tisa watoto watafanya mtihani na wapo watakao chaguliwa hivyo ni lazima waanze maandalizi ya kuwapokea mapema kuanzia mwezi wa pili sambamba na kuwapongeza kwa ujenzi wa kituo cha afya.


Baada ya mkuu wa mkoa wa dodoma dk mahenge kufika katika halmashauri hiyo pia alikuta kuna changamoto ya madawati hivyo akaamua kuwachangia fedha kiasi cha sh million mbili na laki tano na hapa mkuu wa wilaya ya kongwa Deogratias Ndejembi anamshukuru dk mahenge kwa kutembelea miradi yao katika Nyanja ya elimu na sekta ya kilimo na kwa kuwapatia madawati yenye thamani hiyo ya pesa.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.