Header Ads

Idriss Amzika Bibi Yake Aandika Waraka Mzito Baada ya Mazishi

Idriss Amzika Bibi Yake Aandika Waraka Mzito Baada ya Mazishi
MSANII maarufu wa vichekesho (comedy) Bongo, Idris Sultan amejikuta akiandika waraka mzito kwa mashabiki wake kuhusu maisha yake baada ya kumaliza kumzika bibi yake aliyefariki na kuzikwa mkoani Tanga.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Idris ambaye juzi alipost picha nyeusi na kuandika Inna lillahi wainna illaihi raji’un 🖤bila kusema nani yake aliyefariki, leo ameweka ujumbe huu.Wakati namzika bibi yangu jana (Allah amrehem), ilipofika wakati huo hapo kwenye picha nikaanza kuwaza. Unakuja duniani unafikia umri wa kuweza kutafakari nini ufanye na maisha yako, unaanza kupelekeshwa na wanaadam ufanye wanayotaka wao, unaamka kila siku cha kwanza unafanya ni kuangalia kwenye simu yako, usipokuta message unaumia kwasababu unahitaji kujua wamekufikiria,Unaingia instagram unakuta likes chache unahisi haukubaliki na hii dunia unahitaji kubadilika ili wakupende, unaanza kuangalia wanaopendwa wanafanya nini ili uige, unatafuta njia rahisi ya kupata likes fasta na unaanza kuishi kwa nia ya kuwafurahisha tu wengine kwa vitu wanavyotaka wao(sio wewe).Unafariki, unaongelewa mara 3 Na baada ya hapo unakumbukwa na ndugu yako mmoja au wawili. Wewe binafsi hauna kweli kitu chako cha tofauti kukiweka kwenye dunia hii ? … Nakumbuka wakati naanza Comedy watu walisema huyu anafanya nini sasa ? Kipindi hicho comedy ni ya Ze Comedy, Futuhi na maigizo ya lafudhi na kuvaa manguo na kujipaka rangi hivyo tu.

Unasahau kuwa katika kipindi flani duniani watu walijua dunia ni flat na waliosema ni duara walinyongwa, ila ona sasa aibu yetu. Kuwa tofauti haimaanishi unakosea, inamaanisha unahitaji mda kuweza kujua njia ipi nyepesi zaidi kufikisha unachotaka kufikisha kwa watu. Sasa huyu kijana Idris anakuja anaongea tu alafu anategemea tucheke, anaandika tu alafu anadhani inaburudisha, vitu vya siasa na mambo ya elimu hayachekeshi au current issues.

Miaka miwili baadae baada ya kukaza palepale nikaanza kupata watu 100 mara laki mara milioni na sasa mamilioni yanaelewa ni kitu gani nilikuwa najaribu kufanya. Maswali ni “Unaishi maisha yako au ya mtu mwingine ?” “Wewe ni nani ?”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.