Header Ads

Mbali Skendo inayomkabili R Kelly Apata Show, Kumshika Mkono Laki Nane

Muimbaji R Kelly amechukua headlines kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni hii ni baada ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa wanawake kumuandama lakini tuhuma hizo hazijamzuia kupata shows mbalimbali zenye gharama ya juu.

Kupitia mtandao wa TMZ umeripoti kuwa R Kelly ana mpango wa kufanya show Mjini Ludwigsburg nchini Ujerumani mwezi April mwaka huu 2019 ambapo unaambiwa mauzo ya tiketi yanatajwa kufikia gharama zaidi ya shillingi laki mbili za Kitanzania pia kwa shabiki atakayetaka kusalimiana naye itabidi alipe zaidi ya laki nane za Kitanzania.

Inaripotiwa kuwa promoter wa show hiyo amesema kuwa anafahamu kuhusiana na scandal inayoendelea kuhusu R Kelly nchini Marekani na hivyo amefanya kumtafutia shows nje .

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.