Header Ads

MC Pilipili Ajibu Tuhuma za Kuiba Mwanamke wa Mtu

Mchekeshaji Emmanuel Mathias maarufu kwa jina la MC Pilipili, amefunguka juu ya tuhuma kwamba ametumia pesa kumpata mwanamke aliyemvisha pete na kwamba amempora mwanaume mwenzake.
 
MC Pilipili amesema kwamba ametumia pesa na pia anamhurumia kijana huyo, lakini anaamini atapata mwanamke mwingine kwani wanawake ni wengi Tanzania.
 
“Aisee nampa pole Tanzania inaonesha wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwa hiyo ni rahisi kumpata mwanamke mwingine, kwani ni wengi Tanzania na duniani,” amesema Mc Pilipili.
 
Mc Pilipili amemchumbia msichana anayejulikana kwa jina la Philomena Thadey maarufu kama Cute Mena, na baada ya muda mfupi zikaibuka tuhuma mitandaoni kuwa alikuwa mchumba wa mwanaume mwingine.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.