Header Ads

Mlipuko watokea katika tanuri moja mjini Paris

Mlipuko uliotokea katika tanuri moja mjini Paris umesababisha watu wengi kujeruhiwa.

Katika maelezo yaliotolewa na kiongozi wa Usalama amesema, eneo namba 9 mtaa wa Trévise tanuri moja liliwaka moto kisha kulipuka.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Ufaransa katika mlipuko huo watu wengi wamejeruhiwa. Chanzo cha mlipuko huo kinasemekana ni kuvuja kwa gesi.

Majengo yanayozunguka eneo la mlipuko yamevunjika vioo, nataswira inaoyoonekana ni kama eneo la vita.

Mpaka sasa polisi hawajazungumza kutoa chanzo rasmi cha mlipuko huo, kwani inazaniwa pia linaweza kuwa ni tukio la kigaidi, uchunguzi bado unaendelea.

Eneo hilo la tukio limefungwa kwa uchunguzi, na vikosi vya uokoaji na utafutaji vimetumwa eneo la tukio.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.