Header Ads

Mtoto wa Rais Trump atajwa kugombea nafasi ya urais wa Benki ya Dunia

Imefahamika kwamba Ivanka Trump binti wa rais wa Marekani, Donald Trump,ni moja ya majina yanayotajwa kuwania nafasi ya rais ya benki ya dunia (WB).

Gazeti la Financial Times limeripoti kwamba baada ya rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim, kujiudhuru kazi hiyo. Katika watu wanaotajwa kuitaka nafasi hiyo ni pamoja na binti wa rais wa Marekani Ivanka Trump, pamoja na balozi wa kudumu wa Marekani katika umoja wa mataifa aliyemaliza muda wake Nikki Haley. wengine ni pamoja na rais wa wakala wa maendeleo wa Marekani Mark Green pamoja na mshauri wa masuala ya kimataifa wa Hazina ya Marekani David Malpass.

Tangu benki hiyo ianzishwe mpaka hivi sasa Marekani kama mwanahisa mkubwa wa benki ya dunia ndio humchagua rais wa benki hio.

Jim Yong Kim ametangaza kwamba ataachia madaraka ifikapo February 1. Alianza kuitumika benki hiyo kama rais mnamo Julai, 2012. Mwaka 2017 aliteuliwa kwa tena kuwa rais wa benki hiyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.