Header Ads

Mzee Yusuf “Mke Wangu Ndio Alipambana Sana na Majambazi”

“Mke Wangu Ndio Alipambana Sana na Majambazi”- Mzee Yusuf
Aliyekuwa Msanii mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Mzee Yusuf ameibuka na kuelekeza mkasa uliompata yeye na mke Wake Leyla Rashid ambao walivamiwa na majambazi nyumbani kwao mapema Wiki hii.

Gazeti la Amani linaripoti kuwa Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu nyumbani kwake Chanika ambapo majambazi hao walivamia na kufanya umafia ikiwemo kumjeruhi Leila sehemu mbalimbali za mwili wake..

Kwenye mahojiano na Gazeti hilo Mzee Yusuf alikiri kuvamiwa na mkewe ndiye aliyejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na ujasiri aliokuwa nao wa kupiga na majambazi:

Ni kweli nimekumbwa na majanga ya kuvamiwa na majambazi na hivi tunavyoongea (Jumatatu iliyopita) niko hospitali hapa Chanika nahangaika na hali ya mke wangu ambaye ameumia.

Unajua baada ya kuvamiwa mke wangu aliwaonesha upinzani mkali kwa kupambana nao hivyo walivyomuona mbishi walimpiga sana nondo za kichwani, mbavuni na mapajani wakati huo mimi nikipambana na jambazi mmoja kule nje ambaye naye alikuwa na bastola lakini niligundua ni zile zinazotumika kupigia baruti“.

Baada ya tukio hilo Leila alipelekwa hospitali ambako alilazwa Baada ya majeraha aliyopata katika tukio hilo Lakini Mpaka hivi sasa ameshatoka hospitali na anaendelea vizuri.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.