Header Ads

Nandy-Siri ya mafanikio yangu inatokana na juhudi zanguKUTOKANA na habari kwamba mafanikio yake ya ghafla yanatokana na mwanaume anayemmiliki kwa sasa, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ ameibuka na kuanika siri iliyo nyuma ya mafanikio yake.  Akizungumza na Mikito Nusunusu, Nandy ambaye anamiliki magari manne ya kifahari na ameweza kuwajengea wazazi wake mjengo wa kifahari alisema hakuna mwanaume yeyote anayemuwezesha kama watu wanavyodai, bali mafanikio yake ni juhudi zake katika kazi pia menejimenti aliyonayo ipo makini ndiyo maana amefika hapo alipo.

“Siri ya mafanikio yangu inatokana na juhudi zangu. Pia nina menejimenti nzuri ambayo ipo siriazi sana linapokuja suala la kazi, ndiyo maana imenifanya niwe na mafanikio haya na hivi karibuni natarajia kufungua kampuni yangu mwenyewe ila siwezi kusema ni ya nini kwa sababu kuna mambo ambayo bado tunayaweka sawa, yakikamilika basi kila mtu atajua,” alisema

STORI: Shamuma Awadhi

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.