Header Ads

Ommy Dimpoz Ampiga Mkwala Mzito Baba yake Mzazi Kuhusu Ugonjwa Anaoumwa

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amempiga mkwara mzito baba’ke, Faraji Nyembo kisa kikitajwa ni ugonjwa wake.  Chanzo makini kutoka Sumbawanga anakoishi mzee huyo kilieleza kwamba Dimpoz alimtumia ujumbe baba yake huyo na kumpiga mkwara mzito kuwa kuanzia sasa asizungumzie kuhusu afya yake au mambo yoyote yanayomuhusu.

“Unajua baba Dimpoz ni muongeaji sana, huwa hapendi kuficha mambo sasa ile anavyozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mwanaye huyo kumbe ilikuwa inamkera hivyo amempiga mkwara mzito kwamba kuanzia sasa asizungumze chochote kuhusu yeye. “Hii inatokana na kwamba Dimpoz hataki watu wajue kuhusu afya yake vile anavyoumwa kwa hiyo anaona baba yake kama anamuharibia wakati alitaka kuufanya ugonjwa huo kuwa siri, ndiyo maana amepata hasira,” kilisema chanzo.


Baada ya kupata habari hizo, Risasi Jumamosi lilimsaka baba Dimpoz kwa njia ya simu ambapo alifunguka kuwa ni kweli amepata ujumbe huo mzito ambao umemuhuzunisha kwani hakutarajia ingekuwa hivyo. “Dimpoz amemtumia mtu ujumbe aniletee mimi kwamba kuanzia sasa siruhusiwi kuzungumza chochote kuhusiana na yeye hivyo nimenawa mikono kwa kweli sasa.

“Nilikuwa namzungumzia kwa uzuri tu mwanangu na kumtetea kwa wale wanaomsema vibaya lakini kaona nilikuwa nafanya vibaya, nimekubaliana naye kwa kuwa hata hainisaidii kitu chochote katika maisha yangu,” alisema baba Dimpoz. Alipotafutwa Dimpoz kwa njia ya simu kwa kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa kuwa yupo Kenya, iliita bila kupokelewa

STORI: Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.