Header Ads

Rais Shein aeleza sababu ya Rais Magufuli kutohudhuria Maadhimisho ya Mapinduzi Zanzibar

Rais Shein aeleza sababu ya Rais Magufuli kutohudhuria Maadhimisho ya Mapinduzi Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza sababu ya Rais wa Jahmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutohudhuria
Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar.

Akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo, Rais Shein amesema kuwa Rais Magufuli ameshindwa kufika kutokana na kupata dharura.

"Hayupo hapa kwa sababu ya dharura aliyonayo kwa hiyo hakuwezi kuhudhuria na ametaka niwape taarifa hiyo naye anatutakia sisi kila la kheri kwenye sherehe zetu hizi," amesema Rais Shein.

Ameendelea kwa kusema taarifa hiyo ya dharura amepatiwa na Rais Mstaafu wa awali ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.