Header Ads

Rais wa Georgia kuutoa sadaka mshahara wake

Rais wa Georgia Salome Zurabishvili atautoa mshahara wake wote kwa taasisi mpya ya kujitolea itayoundwa na ofisi ya rais.

Zurabishvili,  ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alikuwa akizungumzia hatua alizochukua baada ya kufutwa kwa fuko la akiba lilikuwa chini ya ofisi ya rais.Hivyo alisema katika kutatua changamoto hiyo ataunda taasisi nyingine ambapo mshahara wake wote utakuwa ukienda huko.

Zurabishvili, alisema kutoa sadaka na kuchukua hatua ni vitu vinavyotakikana hivyo yeye kama rais na mtetezi wa mambo hayo kwa niaba yake na wafanyakazi wa umma itaundwa taasisi mpya. Na mwanzo ataanza kwa kujitolea mshahara wake kwa taasisi hiyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.